Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, kufuatia mabadiliko ya hivi karibuni huko Ghaza, Baraza la Umoja wa Waislamu Pakistan lilifanya maandamano makubwa katika jiji la Karachi, Pakistan, kwa ajili ya kuunga mkono watu wa Palestina waliozuiwa na kuulaani kwa nguvu uhalifu wa utawala wa Kizayuni wa Israeli.
Katika mkutano huo, Hujjatul Islam Sayyid Hasan Zafar, Katibu Mkuu wa Baraza la Umoja wa Waislamu Pakistan, akitaja matukio ya hivi karibuni Ghaza, alisema: Marekani na utawala wa Israeli wameshindwa katika vita hii na ushindi wa mwisho ni wa taifa la Palestina na upande wa muqawama. Kusimama kwao na umoja wa ummah wa Kiislamu hatimaye kutaweka misingi ya uhuru wa mji mtukufu wa Quds na kusababisha kushindwa nguvu zote za uvamizi.
Aliongeza katika hotuba yake kuwa: tunatoa sapoti kamili kwa msimamo na maamuzi ya taifa la Palestina, hasa harakati ya Hamas, katika mchakato wa amani Ghaza. Mpango unaojulikana kama “Mpango wa Karne” au “Mradi wa Trump” ni njama hatari dhidi ya haki za msingi za taifa la Palestina. Enzi ya unyonyaji wa Marekani duniani inazidi kupungua, na Washington na Tel Aviv hawatowahi kufanikiwa kutekeleza malengo yao ya kikoloni katika Mashariki ya Kati. Hatima ya Palestina inapaswa kuamuliwa na watu wa ardhi hiyo wenyewe pekee.
Wahubiri wengine katika mkutano huo pia walisisitiza umuhimu wa serikali ya Pakistan kuliunga mkono suala la Palestina na kusema: kuunga mkono sera za Marekani na serikali yake ya awali ni usaliti kwa azma ya Palestina na ummah wa Kiislamu. Serikali ya Pakistan inapaswa kuwa wazi na kushikamana kwao kabisa na muqawama wa Palestina na hasa harakati ya Hamas. Nchi nyingine za Asia hazitaruhusu njama za ukoloni za Marekani na Israeli zitekekezwe katika eneo hili. Utawala wa Kizayuni wa Israeli kwa miaka mingi umekuwa ukiendesha siasa za uvamizi; umekuwa ukifanya mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita dhidi ya watu wa Palestina, na ni muhimu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iwafikishe mbele ya sheria viongozi wa utawala huo kwa makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya utu.
Wahubiri pia walisisitiza kwamba watu wa Pakistan wataendelea kusimama pamoja na taifa la Palestina na hawatawaacha ndugu zao pekee katika njia hiyo. Israel ni utawala usio halali na mwizi, na msimamo thabiti wa wazazi wa Pakistan katika kukataa utawala huo unaendelea kuwa chanzo cha msukumo kwa taifa letu. Watu wa Pakistan wanakataa mpango wa pande mbili na hawataitambua Israeli kamwe. Ummah wa Kiislamu unapaswa kuwa na umoja na tahadhari dhidi ya njama hii inayolenga kuondoa utambulisho, uhuru na umoja wa kijiografia wa taifa la Palestina.
Mwishoni, wahubiri walitoa onyo kwamba Serikali ya Pakistan haipaswi kutafuta kuiridhisha Marekani kwa kuanza mchakato wa kawaida wa mahusiano na utawala wa Israeli, na ilipaswa kukataa mara moja sera za Marekani zinazoikandamiza Palestina na mpango unaoitwa “Mpango wa Karne”.
Maandamano hayo yalifanyika kwa ari kubwa na maulama wengi walishiriki, wanaharakati wa kisiasa na tabaka mbalimbali za jamii, na kaulimbiu zisemazo “Palestina itashinda!” na “Kifo kwa Israeli!” zilirudiwa katika mitaa ya Karachi.
Maoni yako